Mke wa Rais wa Marekani Melania Trump, amekanusha kuwa na uhusiano na Jeffrey Epstein, akiwaambia waandishi wa habari katika Ikulu ya White House kwamba madai yoyote yanayowaunganisha wawili hao “yanahitaji kumalizika haraka”.
Kupitia kwa tangazo siku ya Alhamisi, Melania alitoa wito wa vikao vya bunge kwa ajili ya manusura wa biashara haramu ya ngono iliyoendeshwa na Epstein.
Pia alikanusha uvumi mtandaoni kwamba Epstein alimtambulisha kwa Donald Trump, akiuita madai hayo kuwa ya kumharibia jina.
Hata hivyo sababu zake za kutoa tangazo hilo, bado hazijabainika.
Hakukuwa na dalili yoyote kutoka ofisini kwake kwamba atatoa taarifa kuhusu Epstein, na Ikulu ya White House haikushirikisha mada hiyo mapema.
Alisema hakuwa mwathirika wa Epstein, ambaye “alikutana naye” kwa muda mfupi tu mwaka wa 2000.
“Sijawahi kuwa na ufahamu wowote kuhusu unyanyasaji wa Epstein dhidi ya waathiriwa wake,” alisema. “Sijawahi kushiriki katika nafasi yoyote. Sikuwa mshiriki.”
Pia alikana kumjua Ghislaine Maxwell, mshirika wa Epstein aliyefungwa jela.
Taarifa ya BBC