Vitambulisho 400,000 havijachukuliwa

Dismas Otuke
1 Min Read

Wizara ya uhamiaji imesema kuwa zaidi ya vitambulisho 400,000, havijachukuliwa na wenyewe kote nchini.

Katibu katika wizara uya uhamiaji Belio Kipsang amesema vitambulisho ni vya wale waliotuma maombi kwa mara ya kwanza na wengine wakibadlisha vile vilivyopotea.

Kipsang amesema kuwa wamekuwa wakitembea kila kaunti kuwashawishi wananchi kuchulua vitambulisho vya vilivyochapishwa.

Aliongeza kuwa wanafanya uhamasisho kupitia kwa Machafu na Manaibu wao ili kuwahimiza waliotuma maombi ya vitambulisho kuchukua stakabadhi zao.

Kipsang ameongeza kuwa tayari wamezuru zaidi ya kaunti 30 nchini kuwahimiza wananchi kuchukua vitambulisho vyao.

Share This Article