Chande aelezea kwanini Tume ya kuchunguza ghasia za uchaguzi Tanzania iliongezewa muda

KBC Digital News
1 Min Read
Jaji Mohamed Chande

Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya vurugu za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 na baada ya uchaguzi nchini Tanzania Jaji Mohamed Chande ametaja sababu nne za tume hiyo kuongezewa muda wa siku 21.

Jaji Chande ametaja sababu za kuomba nyongeza hiyo ya muda kuwa ni ukubwa, kina kwa kazi hiyo na ushahidi uliochelewa kuwafikia na ripoti hiyo kutakiwa kuandikwa kwa lugha mbili ya Kiswahili na Kingereza.

“Moja ushahidi mwingi unaendelea kuja, pili ushauri wa kitaalamu ambao tumeuomba wataalamu wa sayansi wanatupa, tatu kuchambua kwa kina, nne kuhakikisha ushahidi huo unakuwa katika lugha mbili za Kiswahili na Kingereza.”

Jaji Chande ameyasema hayo leo Aprili 8, 2026 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam.

Aidha, Jaji Chande amesema kuwa awali walipanga kufanya uchunguzi katika mikoa sita lakini wamelazimika kufikia mikoa 12 na kukusanya taarifa.

Katika hatua nyingine Jaji Othuman Chande amesema kuwa Tume hiyo ni huru,na inafanya kazi zake kwa weledi na haingiliwi katika majukumu yake na hakuna wa kuweza kuwapangia nini chakuandika na kipi cha kuacha .

Share This Article