Wachezaji saba wa timu ya taifa ya Eritrea hawajulikani waliko baada ya kuingia hatua ya makundi ya mechi za kufuzu kwa fainali za Kombe la mataifa ya Afrika mwaka ujao.
Yamkini saba hao walitowekea nchini Eswatini,punde baada ya kuisaidia timu yao kuwashinda wenyeji katika mechi ya marudio tarehe 31 mwezi uliopita mabao 2-1, na kufuzu kwa hatua ya makundi kuwania tiketi ya kushiriki AFCON mwaka 2027.
Eritrea ilisajili ushindi wa jumla wa ambao 4-1 dhidi ya Eswatini katika mchujo huo wa kwanza wa kufuzu AFCON.
Ni wanandinga watatu pekee ;Ablum Teklezgi, Nahom Tadesse,na Rommel Abdu, waliopatikana wakati wa safari ya kurejea nyumbani baada ya mechi.
Sio mara ya kwanza kwa wachezaji wa Eritrea kutoweka kila wanaposafiri nje ya nchini na yamkini huenda waliotoweka wakatafuta hifadhi ya wakimbizi.
Fainali za mwaka 2027 za AFCON zitaandaliwa kwa pamoja na mataifa ya Kenya,Uganda na Tanzania.