IEBC:Ni wapiga kura pekee ambao hawakunakiliwa  kieletroniki ambao wanahitaji kujisajili tena

Dismas Otuke
1 Min Read
Wakenya 90,020 wamesajiliwa kuwa wapiga kura kwenye zoezi linaloendelea la usajili wa wapiga kura kote nchini.

Tume huru ya uchaguzi na uratibu wa mipaka nchini (IEBC ),imefafanua kuwa ni wapiga kura pekee ambao walisajiliwa kabla ya mwaka 2012, na ambao hawakunakiliwa keieltroniki wanaopaswa kujisajili tena kwenye zoezi la usajili linaloendelea.

Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari IEBC imesema  kamwe haifanyi usajili upya wa wapiga waliokuwa wamesajiliwa awali.

Imeongeza kuwa inatumia sajili ya mwaka 2013 ambayo ilitoa shurti la  kuwa na takwimu za wapiga kura kwa njia ya kielektroniki.

Haya yanajiri wakati kumewa na uvumi unaozagaa kuwa IEBC inafanya usajili upya wa wapiga kura waliokuwa wamesajiliwa kabla ya mwaka 2012.

Share This Article