Polisi wachangia damu Kisii

Dismas Otuke
1 Min Read

Katika tukio lisilo la kawaida maafisa wa polisi katika kaunti ya Kisii, siku ya Ijumaa walishiriki zoezi la kutoa damu hafla iliyoendeshwa na wanafunzi kutoka hospitali ya mafunzo  na rufaa ya Kisii.

Damu hiyo itatumika kuokoa maisha ya wagonjwa  wanaohitaji ongezeko la damu katika hospitali ya Kisii wakimiwemo majeruhi wa ajali,wanawake wanaojifungua na wagonjwa wa Selimundu.

Ilikuwa hatua ya ukarimu na dhihirisho la utu kutoka kwa maafisa wa polisi kuitikiwa wito huo.

Share This Article