Mabingwa watetezi wa Ligi kuu ya Kenya ,Police FC walipata ushindi wa bao moja kwa bila dhidi ta Tusker FC,katika moja kati ya mechi mbili za Ligi zilizosakatwa Ijumaa katika uwanja wa Police Sacco.
Goli la pekee na la ushindi kwa Maafande lilipachikwa kimiani na mshambulizi wa Burkina Fasso Yves Koutiama, katika dakika ya 63.
Katika pambano jingine Sofapaka FC waliendelea kutapatapa baada ya kushikwa mateka nyumbani wakiambulisa sare tasa dhidi ya Bandari FC.