Halmashauri ya Ukusanyaji Ushuru nchini, KRA imeanzisha mfumo wa kujaza fomu za kulipia ushuru kupitia kwa mtandano wa WhatsApp.
Kamishna Mkuu wa KRA Humphrey Wattanga amesema mpango huo ni mojawapo wa mikakati ya kujumuisha mifumo ya kisasa ya kujaza fomu za kulipia ushuru ili kurahisha shughuli hiyo kwa wafanyabiashara wadogo wanaopata changamoto kutumia mtandao.
KRA imeweka makataa ya kujaza fomu za kuthibitisha kulipa ushuru wa mwaka 2025 kuwa Juni 30 mwaka huu na tayari zoezi hilo limengóa nanga.