Ngozi za punda zaidi ya 3,000 zanaswa Kitui

radiotaifa
1 Min Read

Taarifa ya Baniface Kanyali

Timu ya usalama iliyokuwa imeshika doria kwenye barabara ya Thika-Garissa karibu na soko la Kanyonyoo imenasa lori lililokuwa likisafirisha tani 12 za ngozi zaidi ya 3,700 za punda kuelekea mahali pasipojulikana. 

Kulingana na stakabadhi zilizotolewa na dereva wa lori hilo lenye nambari ya usajili KBJ 165S, ngozi hizo zilitoka Turkana na zilidaiwa kusafirishwa hadi Mombasa na kisha China.

Afisa mkuu wa mifugo katika kaunti ya Kitui Jonathan Kyambi ametoa wito kwa umma kuchukua tahadhari na kuripoti visa vyovyote vya kuchinjwa kwa punda katika maeneo yao husika.

Asasi za usalama nazo zimetakiwa kufanya uchunguzi wa kina kuhusiana na zilikotoka ngozi hizo na wahusika wa uovu huo kuwajibishwa.

 

Share This Article