Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji nchini Kenya (KBC) Agnes Kalekye amejumuishwa kwenye kamati ya watu 38 itakayoshughulikia maandalizi ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka ujao.
Kamati hiyo itaongozwa na Katibu Mkuu wa zamani wa CECAFA Nicholas Musonye ambaye pia aliongoza kamati iliyosimamia fainali za CHAN mwaka uliopita.
Musonye atasaidiwa na Rais wa FKF Hussein Mohammed na pia inawajumuisha wachezaji waliostaafu wakiwemo Dan Shikanda na McDonald Mariga ambaye pia ni Naibu Rais wa FKF.
Kamati hiyo imejukumiwa na kusimamia maandalizi yote yakiwemo ya viwanja, mikahawa, na usalama kabla na wakati wa fainali hizo.
Kenya itaandaa fainali za AFCON za mwaka 2027 kwa pamoja na Tanzania na Uganda kati ya Juni 19 na Julai 18.