Katibu Mkuu wa shirikisho la kandanda barani Afrika-CAF, Veron Mossengo Omba, amejiuzulu siku ya Jumapili kutokana na kile alichokitaja kuwa kustaafu kwa hiari.
Hata hivyo, inaaminika kuwa shinikizo kali ndani na nje ya shirikisho zimemlazimu kujiuzulu baada ya kutimu umri wa kustaafu wa miaka 63, miaka mitatu iliyopita.
Veron alitimiza umri wa kustaafu katika CAF mwaka 2022, lakini akaongeza kandarasi ya miaka mitatu zaidi.
Licha ya kutangaza kustaafu, inaaminika kuwa Veron anapania kuwania Urais wa shirikisho la kandanda katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.