KUPPET, walimu wanagenzi waitaka serikali kutii uamuzi wa mahakama

radiotaifa
1 Min Read

Taarifa ya Sayyid Abdalla

Serikali kuheshimu uamuzi wa mahakama na kuwaajiri rasmi walimu wanagenzi mbali na kuwaongezea mishahara ili kujimudu kama wafanyakazi wa serikali.

Wito huo umetolewa na Chama cha Walimu wa Shule za Upili na Vyuo, KUPPET katika kaunti ya Busia pamoja na walimu wanagenzi.

Wakiongozwa na Katibu Mkuu wa KUPPET tawi la Busia Charles Mukhwana, wamesema kuwa ni kinaya kikubwa kwa walimu hao kugharimika na kusomea ualimu kisha kulipwa shilingi elfu 17 kama mshahara kila mwezi.

Wameapa kutorudi shuleni muhula ujao iwapo serikali itapuuza wito wao.

Share This Article