Idadi ya waliofariki kutokana na mafuriko yafika 88

Tom Mathinji
1 Min Read

Watu 88 wamefariki kutokana na mafuriko, huku msimu wa mvua ukiendelea kushuhudiwa kote nchini.

Kupitia kwa taarifa, Huduma ya Taifa ya Polisi imesema kuwa familia 2,690,zimeachwa bila makao na sasa zinaishi katika makao ya muda.

Huduma hiyo imeonya kuwa mvua imeharibu barabara nyingi na kuharibu daraja, na kutatiza shughuli za uchukuzi.

“Mvua inayoendelea imetatiza shughuli za uchukuzi na kuharibu daraja kadhaa na hivyo kuhujumu operesheni za kibinadamu,” ilisema huduma hiyo.

Katika kaunti ya Makueni, mtu mmoja alifariki kutokana na maporomoko ya ardhi, huku watu wanne wakijeruhiwa.

Hata hivyo, huduma hiyo ilihakikishia umma kuwa kundi la asasi mbalimbali liko tayari kutekeleza shughuli za uokoaji, utafutaji na usambazaji misaada.

Share This Article