Iran yakana kushiriki mazungumzo na Marekani

Martin Mwanje
1 Min Read
Rais wa Marekani Donald Trump (Picha kwa hisani ya Andrew Harnik/Getty Images)

Rais wa Marekani Donald Trump amesema kwamba Marekani ilifanya mazungumzo na Iran mwishoni mwa wiki iliyopita.

Akizungumza na wanahabari jana Jumanne jimboni Florida, Trump alidai kuna “mambo makuu ya makubaliano,” na Iran inataka makubaliano “mno.”

Hata hivyo, Iran imepuuzilia mbali madai ya Trump.

Kulingana na Trump, makubaliano hayo yalikuwa na “hoja 15,” na kwamba Iran ilikubali kutomiliki silaha za nyuklia.

Alisema mazungumzo hayo yalifanyika siku ya Jumapili baada ya upande wa Iran kupiga simu, na kwamba mkwewe Trump, Jared Kushner na mjumbe maalum Steve Witkoff walishiriki mazungumzo hayo.

Trump alitangaza kwamba ataahirisha mashambulizi kwa “kipindi cha siku tano” ili kutatua mgogoro huo, la sivyo “ataendelea na mashambulizi ya mabomu.”

Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ilinukuliwa ikisema kwamba hakuna mazungumzo yanayoendelea na Marekani, na kwamba kauli za Trump zinalenga kupunguza bei za nishati na kutafuta muda wa kuratibu mipango ya kijeshi.

Bei za mafuta zimekuwa zikiongezeka duniani kote kufuatia mgogoro unaoendelea Mashariki ya Kati.

Mgogoro huo ulianza baada ya nchi za Marekani na Israel kuishambulia Iran ambayo imekuwa ikijibu mashambulizi hayo na kufanya mgogoro huo kuwa mbaya zaidi.

Share This Article