CHADEMA wataka kesi ya Lissu iharakishwe

Wanataka kesi hiyo ikamilishwe ili Tundu Lissu aweze kupata huduma za matibabu.

Marion Bosire
1 Min Read
Kiongozi wa chama cha CHADEMA Tundu Lissu

Wanachama wa chama cha upinzani nchini Tanzania CHADEMA wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche, wameiomba Mahakama iitishe na kusikiliza kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Chama hicho, Tundu Lissu.

Kulingana na Heche, wanataka kesi hiyo iishe na Lissu aruhusiwe kwenda kwa matibabu. Alionya kwamba iwapo Lissu atapatwa na lolote akiwa gerezani kuna Watu watalazimika kujibu kilichompata.

Akiongea Jijini Dodoma leo Machi 24, 2026, Heche amesema kwamba Lissu akiwa gerezani aliandikia Mahakama wa Rufani kwa hati ya dharura kusikiliza kesi dhidi yake ya Uhaini na kuifanyia maamuzi.

“Sote tunajua Lissu alishambuliwa kwa risasi hapa Dodoma kwa hiyo kila baada ya muda amekuwa akienda kwenye matibabu,” alisema Heche.

Aliongeza kusema kwamba suala la afya ya Lissu linahusu Chama na Watanzania.

Heche alisema leo ni siku ya 350 ya Lissu gerezani na amebakisha siku 15 pekee atimize mwaka mzima kwa kile alichokitaja kuwa kesi ya uongo na ya kutunga.

Share This Article