Trump asitisha mashambulizi ya kiwanda cha umeme nchini Iran kwa siku tano

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais Donald Trump wa Marekani amesema leo kuwa ameagiza kusitishwa kwa mashambulizi yaliyopangwa ya kijeshi katika  kiwanda cha kuzalisha nishati nchini Iran kwa siku tano zaidi.

Kupitia kwa mitandao ya kijamii Trump amekiri kuwepo kwa mazungumzo mazuri kwa siku mbili zilizopita kuhusu suluhulu mwafaka ya kumaliza mzozo wa Mashariki ya Kati.

Zaidi ya watu 2,000 wameuawa kwenye mashambulizi hayo nchini Iran yanayoongozwa na majeshi ya Marekani na Israel tangu yaanze Februari 28.

Mashambulizi hayo yamesababisha kuongezeka kwa bei ya mafuta katika eneo la ghuba na bidhaa nyingi za matumizi.

 

 

Share This Article