Klabu ya Kenya Pipeline ilisajili ushindi wa seti 3-1 katika mechi ya kuwania taji la Kenya Cup.
Mchuano huo ulipigwa uwanjani Nyayo.
Pipeline walishinda seti mbili za kwanza alama 25-17 na 25-16, ila wakapoteza ya tatu 24-26, na kuibuka kidedea katika seti ya mwisho kwa alama 25-21.
Mechi hiyo ilikuwa ya raundi ya pili katika makala ya pili ya mashindano ya Kenya Cup.