Rais William Ruto siku ya Jumamosi amezindua ujenzi wa miradi kadhaa ya maendeleo ya kima cha shilingi bilioni 28, katika kaunti ya Siaya.
Miradi hiyo inajumuisha ujenzi wa nyumba za gharama nafuu, masoko ya kisasa na vyumba vya kulala kwa wanafunzi.
Ruto ameweka jiwe la msingi kwa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu eneo la Yala, eneo bunge la Gem kwa gharama ya shilingi milioni 800.