Katibu katika Wizara ya Mambo ya Nje Korir Sing’Oei, amesema kuwa ili bara la Afrika liweze kukabilina na changamoto zilizopo, ni sharti liweze kuzungumza kwa sauti moja.
Akizungumza leo Alhamisi alipokuwa mwenyeji wa maafisa wa kidiplomasia, katibu huyo alidokeza kuwa umoja wa Afrika unapaswa kuzingatia amani ya kikanda, uhuru wa mataifa na utumizi wa kawi safi kwenye viwanda.
“Siku zilizosalia za mwaka 2026, zinaashiria msimu muhimu wa kutekeleza uchumi wa kidiplomasia wa taifa hili,” alisema Sing’Oei.
Aidha aliongeza kuwa ili kuhakikisha upatikanaji wa soko la watu bilioni 1.4 wa bara Afrika, ni muhimu kuondoa vikwazo vya ushuru katika kanda ya EAC na kutekelezwa kwa mifumo ya kidijitali ya kibiashara.
“Mustakabali wa Afrika utatekelezwa na hatua za kijasiri na jumuishi zinazotumiwa leo,” alisema katibu huyo.