Rais wa CAF akubali uamuzi wa bodi ya rufaa kuipokonya Senegal kombe

Dismas Otuke
1 Min Read
Patrice Motsepe

Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), Patrice Motsepe, amesema amekubali uamuzi wa Jumanne wiki hii wa bodi ya rufaa kuipokonya Senegal ubingwa wa AFCON na kuitwika Morocco.

Motsepe amesema anaheshimu uhuru wa kamati huru ndani ya CAF na pia haki za mataifa yote 54 wanachama wa shirikisho hilo.

Aidha, amesema pia ataunga mkono na kukubali uamuzi wa mahakama ya kimataifa ya kutatua migogoro ya michezo (CAS) baada ya Senegal kuashiria kuwa itawasilisha kesi kupinga uamuzi wa kuipokonya kombe.

Share This Article