Raia wa Qatar waagizwa kuhamia maneno salama

Tom Mathinji
1 Min Read

Raia nchini Qatar wameagizwa kuhamia maeneo salama, huku mzozo ukiendelea kughubika Mashariki ya Kati.

Tahadhari hiyo imetolewa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Qatar, ambayo ilisema hiyo ni hatua ya muda hadi hali ya usalama itakaporejea.

Hali sawia na hiyo imetangazwa nchini Bahrain, ambayo iliwataka raia wake kujificha baada ya ving’ora kulia, huku Saudi Arabia pia ikisema imezuia makombora kadhaa.

Hayo yanajori huku Iran ikionya kushambulia miundombinu ya mafuta ya washirika wa marekani, iwapo miundombinu yake itashambuliwa.

Vikosi vya Israel na Marekani vimetekeleza mashambulizi ya kijeshi nchini Iran, Tehran pia ikitekeleza mashambulizi Israel.

Vita hivyo hadi sasa vimedumu wiki mbili.

TAGGED:
Share This Article