Idadi ya waliofariki kutokana na mafuriko yafika 62

Tom Mathinji
1 Min Read
Idadi ya waliofariki kutokana na mafuriko yafika 62.

Idadi ya watu waliofariki kutokana na mafuriko hapa nchini imefika 62, hayo ni kulingana na Wizara ya Mambo ya Ndani.

Kupitia kwa taarifa Ijumaa alasiri, wizara hiyo iliongeza kuwa idadi hiyo ilijumuisha wanaume 46, wanawake wanane na watoto wanane.

Kulingana na idadi hiyo, kaunti ya Nairobi iliathirika zaidi huku ikinakili maafa 33 ikifuatwa na eneo la Mashariki iliyonakili vifo 17 nayo Rift Valley ikinakili vifo 7.

Watu wawili walifariki Nyanza na eneo la Pwani kutokana na mafuriko hayo huku eneo la kati likinakili kisa kimoja.

Maeneo mengi ya nchi yanashuhudia mvua kubwa ambayo inasababisha mafuriko, huku Idara ya Utabiri wa Hali ya Hewa ikidokeza kuwa mvua hiyo itaendelea kushuhudiwa katika muda wa siku chache zijazo.

Share This Article