Vita vya vinavyoshuhudiwa vya Marekani na Israel dhidi ya Iran, vinatatiza uuzaji wa bidhaa za Kenya katika eneo la Mashariki ya Kati.
Akithibitisha hayo leo Alhamisi, Waziri wa Kilimo na Ustawi wa Mifugo Mutahi Kagwe, alisema kuwa vita hivyo vimesababisha taifa hili kutouza bidhaa vya thamani ya shilingi milioni 300 kila wiki.
Kulingana na waziri huyo, bidhaa zilizoathiriwa na vita hivyo ni nyama, baadhi ya bidhaa za wanyama, huku kituo cha usambazaji Majani Chai cha Dubai pia kikiathiriwa na mzozo huo ambao sasa umedumu wiki mbili.
Aidha, waziri kagwe aliwahakikishia Wakenya kwamba serikali tayari imechukua hatua mwafaka za kupata masoko mbadala ili kuwalinda wauzaji bidhaa nje ya Kenya.
Kagwe alisema serikali inafanya kila juhudi kudhibiti hali hiyo, huku kundi maalum likiumwa kutathmini athari na kuunda mkakati wa kukabiliana na hali hiyo.