Dereva mmoja wa matatu amenaswa na maafisa wa polisi katika kaunti ya Kisumu akisafirisha bangi.
Polisi waliokuwa wakifanya msako na ukaguzi wa kawaida walilisimamisha gari hilo na kupata misokoto ya bangi iliyokuwa ndani ya magunia mawili.
Bangi hiyo ya uzani wa kilo 90 ilikuwa ikisafirishwa na dereva huyo wa matatu kuelekea mahali pasipojulikana.
Mshukiwa amewekwa korokoroni kusaidi polisi katika uchunguzi.