Kenya na Uingereza zimeimarisha mpango wa pamoja wa kuboresha Jiji la Nairobi uliokitwa kwenye mradi wa uchukuzi wa reli wa jiji hilo.
Mkuu wa Mawaziri Musalia Mudavadi amesema Uingereza inashirikiana na serikali ya Kenya kuboresha uchukuzi wa reli na miundombinu ya barabara, ambao umehamasishwa na mfumo wa uchukuzi nchini Uingereza.
Akizungumza jijini London, Uingereza, Mudavadi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje, alielezea hatua zilizopigwa katika kuwatafuta wataalam na wanakandarasi wa mradi huo ambao unalenga kufungua fursa za kiuchumi kwa jiji hilo.
Mudavadi aliyasema hayo wakati wa Mkutano wa 26 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola nchini Uingereza.
Wengine waliohudhuria mkutano huo ni Kaimu Balozi wa Uingereza nchini Kenya na Balozi wa Kenya nchini Uingereza Maurice Makoloo.