Mwakilishi wa eneo bunge la Kitui Kusini bungeni Rachel Kaki Nyamai, amehimiza wanawake walio katika nafasi za uongozi wakumbuke wanawake mashinani.
Kulingana na kiongozi huyo, wanawake na hasa kina mama wanateseka vijijini na wanastahili kuwasaidia kujikwamua. Aliomba pia usaidizi kwa wanawake wanaoathiriwa na unyanyasaji wa kijinsia.
Mbunge huyo alisema kwamba wakati huu ambapo wanawake wanaenziwa ulimwenguni kote, ni muhimu kwa wanawake kuchukua hatua na kuhusika katika uongozi.
Alisisitiza kwamba wanawake wanafaa kupatiwa fursa sawa na wanaume katika nyadhifa fulani za uongozi ili waweze kukua na kuchangia katika ukuaji wa jamii.
Nyamai aliwataka wazazi pia wawe wakifuatilia watoto wao wakati huu wa mvua nyingi ili kuwakinga kutokana na hatari zinazoweza kutokea kama ajali.