Watu watatu walithibitishwa kuaga dunia kufuatia ajali ya Jana Jumapili, iliyohusisha gari la Tuk tuk na gari la maafisa wa usalamala wa Waziri Wa Afya Aden Duale eneo la Otonglo katika barabara kuu ya Kisumu-Busia.
Watu wawili walifariki papo hapo huku mwingine mmoja akifariki katika hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga, alipokuwa akipokea matibabu.
Duale alikuwa njiani kuelekea Rarieda kaunti ya Siaya, kutoka uwanja wa Ndege Wa Kisumu kuhudhuria ibada ya shukran ya Katibu Wa huduma za Afya Ouma Oluga iliyoonozwa Na Rais William Ruto.