Mtandao wa kuchagua kozi kwa wanafunzi wa vyuo na taasisi za kiufundi nchini KUCCPS umefunguliwa Jumapili kwa wanafunzi wanaotaka kujiunga na vyuo vya TVET kote nchini mwezi Mei.
Wanafunzi waliokalia mtihani wa kidato cha nne mwaka 2025 wako huru kutuma maombi ya kozi zinazotolewa na vyuo vya kiufundi vya kitaifa.
Maombi kwa kozi hizo yatafungwa ifikiapo Machi 18, huku watakaofaulu kuteuliwa wakijiunga na vyuo vya kiufundi mwezi Mei mwaka huu.