Wizara ya Afya imekiri kuwepo kwa uhaba wa chanjo ya Rotavirus humu nchini inayotolewa kwa watoto walio na umri wa wiki 6, 10 na 14.
Kampuni ya Gavi inayosambaza chanjo hiyo ilifahamishwa na watengenezaji wa chanjo Bharat Biotech, kuhusu upungufu wake kutokana na ukarabati wa upanuzi wa kiwanja unaofanyika baina ya mwaka huu na mwaka ujao.
Kulingana na Wizara ya Afya, kufikia Machi 3 mwaka huu, Kenya ilikuwa na akiba ya dozi 4,000, za chanjo ya Rotavirus, ambazo zinatumika chini ya mwezi mmoja.
Shehena ya chanjo hiyo iliyokuwa iwasilishwe nchini mwezi Januari mwaka huu ilichelewa na huenda ikawasili mwishoni mwa mwezi ujao.