Rais Ruto akutana Ikuluni na Waakilishi 40 wa bunge la Kitui

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto mapema Ijumaa amekutakana na waakilishi wa bunge la Kitui, katika Ikulu ya Nairobi na kujadiliana kwa kina kuhusu upigaji jeki wa miradi ya maendeleo katika kaunti hiyo.

Waakilishi hao wakiongozwa na Spika wa bunge hilo, Kevin Kinengo Katisya, walijadiliana na Rais kuhusu miradi kadhaa ya maendeleo, ikiwemo uunganishwaji umeme, nyumba za gharama nafuu, ujenzi wa masoko ya kisasa, ujenzi wa barabara, ujenzi wa mabwawa ili kumaliza ukosefu wa maji na utoaji wa hati miliki za mashamba.

Share This Article