Mhubiri anayekumbwa na utata Paul Nthenge Mackenzie, pamoja na washukiwa wengine saba, walifikishwa katika Mahakama moja ya Mombasa kufunguliwa mashtaka kadhaa ya mauaji kuhusiana na maafa katika shamba la Binzaro kunti ya Kilifi.
Mackenzie na washukiwa hao ambao ni Shallyne Anindo Temba almaarufu Ann, Kahindi Kazungu Garama almaarufu Mlewa, Tom Ochieng Mkonwe almaarufu Thomas au Tomaso, Julius Tuva Luwali, Johnson Gona Richard, Charles Mutua Musee almaarufu Mzee Mutua, na James Kazungu Kahindi almaarufu Ponda au Baba Bura, watajibu mashtaka ya uhalifu dhidi ya binadamu.
Wanashtumiwa kwa kutekeleza mashambulizi haramu yaliyosababisha kuuawa kwa wanachama 23 na wafuasi wa kanisa la Good News International, waliokuwa na umri wa kati ya miaka sita na 18.
Justice Wendy Kagendo,alifahamishwa kuwa jinsia za waliofariki hazikuweza kubainishwa wakati wa uchunguzi.
Visa hivyo vinadaiwa kutekelezwa kati ya mwezi Januari na Julai mwaka 2025 katika eneo la Kwa Binzaro, kaunti ndogo ya Magarini, kaunti ya Kilifi.
Hata hivyo, washukiwa hao wanane walikanusha mashtaka hayo.
Justice Kagendo aliagiza kuwa Mackenzie azuiliwe rumande katika gereza la Shimo la Tewa Prison, huku washukiwa wenzake saba wakizuiliwa katika gereza la Malindi kwa muda wa wiki mbili, wakisubiri kuhamishwa katika gereza la Shimo la Tewa.
Upande wa mashtaka umedokeza kuwa unalenga kuwasilisha mashahidi 128 na ushahidi kadhaa kupiga jeki kesi hiyo