Tubi Mohamed, aapishwa kuwa Mbunge wa Isiolo Kusini

Dismas Otuke
1 Min Read

Tubi Mohamed Tubi wa chama cha United Democratic Alliance (UDA) amekula kiapo Alhamisi Alasiri kuwa mbunge wa eneo bunge la Isiolo Kusini.

Tubi aliye na umri wa miaka 36, alitangazwa mshindi wa uchaguzi mdogo ulioandaliwa tarehe 26 mwezi uliopita baada ya kuzoa kura 7,352, dhidi ya mpinzani wake Bina Mohamed wa Jubilee aliyepata kura 634.

Kiti hicho kiliachwa wazi kufuatia kifo cha Mohamed Tubi Bidu, Novemba 12, mwaka jana, katika Hospitali ya Nairobi baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Share This Article