Kibet kuongoza timu ya Kenya kwa mashindano ya Dunia ya ukumbini

Dismas Otuke
1 Min Read

Mshindi wa nishani ya fedha Noah Kibet ataongoza kikosi cha wanariadha sita watakaoiwakilisha Kenya kwenye mashindano ya dunia ya viwanja vya ndani yatakayoandaliwa kati ya tarehe 20 na 22 mwezi huu nchini Poland.

Kibet anarejea baada ya kumaliza wa pili katika mita 800 mwaka 2022.

Wanariadha wengine kikosini ni Susan Ejore atakayetimka mita 1500, Rosemary Longisa mita 800, Mercy Oketch na Brian Tinega mita 400 na Jacob Krop mita 3000.

Share This Article