Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imetangaza kuanza awamu ya pili ya usajili wa wapiga kura tarehe 30 mwezi huu.
Mwenyekiti wa tume hiyo Erastus Ethekon amewataka wanasiasa kuwahimiza Wakenya kujisajili kwa wingi kuwa wapiga kura kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.
Aliyasema hayo kwenye kikao cha pamoja cha shirika la kupigania demokrasia la CMD katika bustani ya Uhuru.
Tangazo la IEBC linakuja wakati ambapo idadi ndogo ya Wakenya walijitokeza kujisajili kama wapiga kura wakati wa zoezi endelevu la kuwasajili wapiga kura.
Kwa kutangaza awamu ya pili ya usajili wa wapiga kura, IEBC imeonekana kuanza maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka ujao unaobashiriwa na wengi kuwa utakuwa na ushindani mkali.