Imam mwenye makao yake eneo la Othaya, kaunti ya Nyeri, amekiri makosa kadhaa ya kuwadhulumu kimapenzi watoto wa umri mdogo.
Iddi Ali Koitat alikiri mbele ya Hakimu Mkuu Sandra Ogot makosa saba ya kuwadhulumu watoto wadogo kimapenzi walio na umri wa kati ya miaka tano na kumi na nne.
Dhuluma hizo zilitekelezwa katika msikiti wa kijamii wa Othaya kati ya mwaka 2022 na mwezi Novemba mwaka 2025.
Wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo katika mahakama ya Othaya, upande wa mashtaka uliomba upewe muda zaidi kuwasilisha ushahidi zaidi kabla ya kuamuliwa kwa kesi hiyo.
Hakimu Ogot alikubali ombi hilo huku akiagiza mshtakiwa kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha Othaya hadi Machi 10, 2026, wakati ambapo mahakama itatoa maagizo zaidi.