Mzozo wa Mashariki ya Kati wasababisha bei za mafuta kuongezeka

Tom Mathinji
1 Min Read
Bei za mafuta zapanda.

Huku taharuki ikiendelea kutanda Mashariki ya kati, bei za bidhaa za petroli zimepanda hasaa baada ya meli tatu  za kubebea bidhaa hiyo kushambuliwa karibu na eneo la Strait of Hormuz.

Kiwango cha kimataifa cha kubaini bei za mafuta ghafi kimeongezeka kwa zaidi ya asilimia 10 hadi zaidi ya dola 82 kwa kila pipa.

Kampuni kubwa ya kiserikali ya mafuta nchini Saudi Arabia, Aramco, imefunga kiwanda chake cha kusafishia mafuta cha Ras Tanura, kufuatia shambulizi  la droni lililohusishwa na taharuki nchini Iran.

Kiwanda hicho cha Ras Tanura kilicho kwenye pwani ya ghuba ya ufalme huo ni mojawapo wa  viwanda vikubwa zaidi vya kusafishia mafuta katika eneo la mashariki ya kati kikiwa na uwezo wa kusafisha mapipa elfu- 550 kwa siku.

Wachanganuzi wanaonya kwamba kuvurugwa kwa shughuli kwenye kiwanda cha Ras Tanura huenda kukapunguza zaidi kiwango cha uuzaji mafuta duniani na kuzidisha bei za kawi na hivyo kuathiri masoko ambayo tayari yanakumbwa na msukosuko.

TAGGED:
Share This Article