Wafanyakazi wa Wizara ya Afya wasaini kandarasi za utendakazi

Dismas Otuke
1 Min Read

Wafanyakazi katika Wizara ya Afya wametia saini kandarasi za utendakazi mwaka 2025/2026 zinazolenga kuboresha utoaji huduma kwa umma.

Waziri wa Afya Aden Duale ameongoza zoezi hilo mapema Jumatatu.

Kandarasi hizo za utendakazi ni za kuanzia Julai mosi mwaka 2025 hadi Juni 30 mwaka huu.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na makatibu Ahmed Abdisalan Ibrahim anayesimamia shughuli za serikali ya kitaifa, Dkt. Ouma Oluga wa huduma za matibabu, Mary Muthoni wa afya ya umma pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Afya, Dkt Patrick Amoth, miongoni mwa maafisa wengine wa wizara.

Share This Article