Mwili wa marehemu mbunge wa Emurua Dikirr Johanna Ng’eno aliyeangamia kwenye ajali ya ndege siku ya Jumamosi umewasilishwa katika chumba cha Lee kaunti ya Nairobi Jumapili alasiri.
Mwili wa marehemu ulipokelewa na wabunge wenza na familia na marafiki waliojawa na simanzi.
Ng’eno alingamia baada ya helikopta aliyokuwa akisafiria kuanguka eneo la Mosop, kaunti ya Nandi.
Hadi kifo chake, marehemu alikuwa amehudumu bungeni tangu mwaka 2013.