Maelfu ya waombolezaji wamejitokeza katikati ya jiji kuu la Iran, Tehran, kuomboleza kifo cha kiongozi Ayatollah Ali Khamenei mapema jana kwenye shambulizi la angani lililotekelezwa na majeshi ya Israel na Marekani.
Waombolezaji hao waliomiminika katika eneo la Enghelab walikuwa wamevalia mavazi meusi huku wakibeba bendera za Iran na mabango yenye picha za Khamenei.
Khamenei, ambaye amekuwa kiongozi wa Iran tangu mwaka 1989 aliuawa mapema Jumamosi.