Rais William Ruto ametuma risala za rambirambi kwa familia na wakazi wa eneo bunge la Emurua Dikirr kufuatia kifo cha Mbunge wao Johana Ngéno, kwenye mkasa wa ajali ya ndege Jumamosi jioni eneo la Mosop kaunti ya Nandi.
Ruto amemtaja kuwa kiongozi mpenda maendeleo na aliyewatumikia watu wa Emurua Dikirr, bila mapendeleo na aliyehimiza ukuzaji wa vipaji hususan usanii wa muziki.
Ngéno ambaye amekuwa bungeni tangu mwaka 2013 alifariki pamoja na watu wengine watano ambao pia waliaga dunia kwenye ajali hiyo ya Helikopta.