Polisi wa eneo la King’eero, kaunti ndogo ya Kabete, walinufaika kwa kupata afisi mpya zilizofunguliwa Ijumaa.
Afisi hizo za kisasa zilifunguliwa rasmi na naibu kamanda wa kaunti ndogo ya Kabete Peter Kimotho, na afisa mkuu mtendaji wa kampuni ya Fireside Rebecca Wanjiku, walifungua afisi hiyo siku ya Ijumaa.
Afisi hizo zilijengwa na kampuni ya Fireside Group Engineering Solutions na zinajumuisha nyumba za naibu OCS, afisi ya kukabiliana na uhalifu na afisi za makosa madogo.