Taarifa ya Jonathan Musau
Hulka za Wakenya zinachangia pakubwa uchafuzi wa mazingira na ipo haja kwao kuzipitia upya ili kufanikisha uwepo wa mazingira safi.
Ni kauli ya wataalamu wa mazingira wakiongozwa na Dkt. Stephen Wambua ambao wameshirikiana na wanafunzi wa vyuo mjini Machakos kufanya shughuli ya usafi mjini humo kwa lengo la kuhamasisha jamii kubadilisha hulka zao ili kuepuka uchafuzi zaidi wa mazingira.
Mpango huu ukipokelewa vizuri na wafanyakazi wa kituo cha mabasi mjini Machakos amboa wameeleza kufurahishwa na kiwango cha usafi kilichoshuhudiwa katika kituo hicho baada ya wanafunzi kujitolea kukisafisha.
Walieleza kuwa ipo haja kubwa ya binadamu kubadili hulka zao hususan utupaji taka kila eneo iwapo kuna ndoto ya kuwahi kuwepo kwa mazingira safi nchini.
Wito ambao umesisitizwa na wahudumu wa matatu baada ya kupokea huduma za usafi kutoka kwa wanafunzi wa vyuo vya mafunzo ya kiufundi mjini Machakos.