Uhuru Kenyatta azuru familia ya hayati Raila

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta leo Jumatatu amezuru familia ya Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga nyumbani kwake Bondo, na kutembelea kaburi la marehemu kutoa heshima zake.

Uhuru aliyekuwa mwandani wa karibu wa hayati Raila aliambatana na kaka mkubwa wa Raila, Oburu Oginga, mjane wa Raila, Ida pamoja na watu wa familia hiyo.

Inaaminika kuwa Uhuru, aliyeshirikiana na Raila kuanzia mwaka 2018 katika serikali yake, alikuwa mwingi wa majonzi alipozuru kaburi hilo huku akikaa kimya kwa muda kutoa heshima zake juu ya kaburi.

Haya yanajiri siku moja baada ya mwili wa Raila kuzikwa nyumbani kwake huko Bondo katika mazishi yaliyoongozwa na serikali.

Share This Article