Lillian Odira amejikakamua na kushinda dhahabu ya mita 800 kwa wanawake katika siku ya mwisho ya makala ya 20 ya mashindano ya Riadha Duniani mjini Tokyo,Japan.
Odira alivunja rekodi ya mashindano hayo ya miaka 40, akitwaa ubingwa kwa dakika 1 sekunde 54.62 .
Uingereza imenyakua fedha na shaba kwa dakika 1 sekunde 54.90 na dakika 1 sekunde 54.91.
Dhahabu hiyo ni saba kwa Kenya ikisalia ya pili kwenye msimamo kwa dhahabu 7 fedha 2 na shaba 2.