Wakenya watahadharishwa dhidi ya upepo mkali utakaovuma katika sehemu kadhaa za nchi

Tom Mathinji
1 Min Read
Mkurugenzi wa Idara ya Utabiri wa hali ya hewa nchini Dkt. David Gikungu.

Idara ya Utabiri wa Hali ya Hewa hapa nchini, imetoa tahadhari kuhusu kuvuma kwa upepo mkali katika sehemu kadhaa za taifa hili.

Baadhi ya kaunti ambazo zitaadhiriwa na upepo huo ni pamoja na Marsabit, Turkana, Samburu, Isiolo, Mandera, Wajir, Garissa, Kitui, Makueni, Taita Taveta, Tana River, Lamu, Kilifi, Mombasa na Kwale.

Hayo yalithibitishwa na Murugnzi wa idara hiyo Dkt. David Gikungu, katika mahojiano na Shirika la Utangazaji Nchini KBC.

“Upepo huo mkali unatarajiwa katika Pwani ya Kenya, nyanda za chini za Kusini Mashariki na Kaskazini Magharibi mwa nchi Ijumaa Mei 23, Jumaosi Mei 24 na Jumapili Mei 25, 2025,” alisema Dkt. Gikungu.

Mkurugenzi huyo ametoa wito kwa wakazi wa maeneo hayo kuwa waangalifu zaidi dhidi upepo huo pamoja na mawimbi makali katika Bahari Hindi.

Wale wanaojihusisha na shughuli za bagarini pia wametakuwa kuchukua tahadhari, kwa kuwa mawimbi makali yatapunguza uwezo wa kuona vyema na hivyo kuhujumu shughuli za baharini kuanzia Ijumaa.

Share This Article