Chama tawala nchini Uganda, National Resistance Movement (NRM), chake Rais Yoweri Museveni, kimeonyeshwa vumbi baada ya kushindwa kwenye uchaguzi mdogo wa eneo bunge la Kawempe kaskazini.
Hii ni baada ya Elias Luyimbazi Nalukoola wa chama National Unity Platform (NUP) kutangazwa mshindi wa uchaguzi huo mdogo ulioandalwia jana.
Nalukoola alipata kura 17,764 akifuatwa na Fariba Nambi wa chama cha NRM kwa kura 8,593.
Chama cha NUP kinaongozwa na mbunge wa zamani ambaye pia msanii Bobi Wine.