Zelensky awashukuru viongozi wa EU kwa kuiunga mkono Ukraine

Tom Mathinji
1 Min Read
Zelensky apongeza EU kwa kuiunga mkono Ukraine.

Rais Ukraine Volodymyr Zelensky, amewashukuru viongozi wa Muungano wa Ulaya kwa kuiunga mkono Ukraine wakati wa mkutano kuhusu usalama wa Baraza la Ulaya mjini Brussels, nchini Ubelgiji.

“Katika kipindi hiki chote, na wiki iliyopita, mumesimama na sisi,” amesema Zelensky.

“Hatuko peke yetu, na haya sio maneno tu, tunahisi.

“Mumeonyesha ishara madhubuti kwa [watu] wa Ukraine,” amesema, na “wanaithamini”.

Hayo yanajiri huku Urusi ikionya dhidi ya wanajeshi wa EU kupelekwa nchini Ukraine.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Urusi  Maria Zakharova,  amesema kwamba matarajio ya kutuma kikosi cha kulinda amani cha Ulaya nchini Ukraine huenda yatazidisha vita.

“Mgogoro utaanza tena kwa nguvu mpya… hili halikubaliki kabisa,” alisema Maria Zakharova.

Amesema wazo la kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Ulaya nchini Ukraine linaonyesha kuwa viongozi wa Ulaya “hawajajifunza kutoka kwa siku za nyuma”.

Zakharova anaongeza kuwa ulinzi wowote wa amani wa Ulaya, iwapo utatokea, “utaumiza” upya utawala wa Kyiv.

Share This Article