Mshikilizi wa rekodi ya Marathon Kelvin Kiptum na bingwa mara mbili wa Olimpiki katika mbio za mita 1,500 Faith Kipyegon, ndio wanariadha bora wa mwaka barani Afrika.
Wawili hao walituzwa na shirikisho la Riadha barani Afrika baada ya kunawiri, Kiptum akishinda mbio za London na Chicago Marathon na kuweka rekodi mpya ya dunia ya saa 2 na sekunde 35.
Kipyegon alihifadhi taji ya dunia ya mita 1,500, akaibuka bingwa dunia katika mita 5,000 na kuvunja rekodi za dunia katika mita 1,500,5,000 na maili moja katika kipindi cha mwezi mmoja.
Patrick Sang alitawazwa kocha bora wa mwaka huku Janeth Jepkosgei akinyakua tuzo ya kocha bora anayeibuka.
Emmanuel Wanyonyi na Faith Cherotich walitawazwa wanariadha chipukizi bora wa mwaka.