Mkenya Edwin Kiprop Kiptoo ametwaa ubingwa wa makal ya 40 ya mbio za Athens Marathon zilizoandaliwa Jumapili nchini Ugiriki.
Kiprop ameziparakasa mbio hizo kwa saa 2 dakika 10 na sekunde 34, akifuatwa na Rhonzas Lokitam kwa saa 2 dakika 12 na sekunde 36.
Sukaina Atanane wa Ethiopia alishinda mbio za wanawake kwa saa 2 dakika 31 na sekunde 53,akifuatwa na Caroline Jepchirchir wa Kenya amechukua nafasi ya pili kwa saa 2 dakika 32 ma sekunde 19.