Wanachama wa Tume ya Kitaifa ya Ardhi wateuliwa

Martin Mwanje
1 Min Read

Dkt. Abdillahi Saggaf Alawy ndiye mwenyekiti mpya wa Tume ya Kitaifa ya Ardhi, NLC. 

Hii ni baada ya kuteuliwa na Rais William Ruto kuhudumu kwenye wadhifa huo kwa kipindi cha miaka sita.

Kwenye gazeti rasmi, Rais Ruto pia amewateua Susan Khakasa Oyatsi, Daniel Murithi Muriungi na Kigen Vincent Cheruiyot kuwa wanachama wa tume hiyo.

Wengine walioteuliwa ni Dkt. Julie Ouma Oseko, Mohamed Abdi Haji Mohamed na Seneta mteule wa zamani Mary Yiane Seneta.

Wote hao pia watahudumu kwa kipindi cha miaka sita.

Uteuzi wao nao unakuja siku chache baada ya kupigwa msasa na bunge.

Share This Article